- 308 viewsDuration: 2:38Kampuni ya M-Ajira imetua jijini Mombasa kuendeleza zoezi la kuwajisajili madereva wa malori kwa nafasi za ajira nchini Saudi Arabia. M-Ajira imeshirikiana na kampuni ya SMASCO kutoka Saudi Arabia kuendesha zoezi hilo kwa siku tatu zijazo katika uwanja wa Tononoka, jijini Mombasa. Zoezi hili linalenga kuwasajili madereva 500 watakaonufaika na nafasi za ajira katika taifa hilo la Ghuba.