- 75 viewsDuration: 1:39Wanaharakati wa uhifadhi wa mazingira wamewataka wananchi kote nchini kuimarisha mshikamano na uwajibikaji wa pamoja katika kulinda ardhi oevu na vyanzo vya maji, ili kukabiliana na uharibifu unaotishia uhai wa binadamu, mimea na wanyama, hasa wakati huu wa ukame unaoendelea kushuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi. Wito huu umetolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ardhi oevu yaliyofanyika katika chemichemi ya Marire, kaunti ya Isiolo.