- 165 viewsDuration: 2:57Ulimwengu leo umeadhimisha siku ya kina mama huku mkewe naibu rais, daktari Joyce Kithure, akiongoza maadhimisho hayo katika makazi yake rasmi eneo la Karen hapa Nairobi. Sherehe hizo za siku nzima zilikuwa za kuwapongeza na kuwathamini kina mama kwa majukumu yao kwa jamii. Haya yameendelea huku wakazi wa Kabarnet kaunti ya Baringo wakijitokeza kumsherehekea mkuu wa polisi wa kituo cha Kabarnet kwa kuongoza juhudi za kumaliza pombe haramu eneo hilo.