- 14,274 viewsDuration: 3:05Mchujo wa vyama vya kisiasa umeendelea kwa siku ya pili katika eneo bunge la Ol Kalou, chama cha DCP kikiandaa zoezi hilo kutafuta mjumbe atakayeperusha bendera ya chama katika uchaguzi wa Julai,16. Zoezi la Jumamosi lilishuhudia idadi kubwa ya wapigakura waliojitokeza kuamua ni nani kati ya wawaniaji tisa atakayetosha kumenyana debeni na Samuel Muchina Nyaga wa UDA na Wilson Kigwa wa chama cha Jubilee.