- 64 viewsMamia ya waandishi wa habari huko pwani chini ya mwavuli wa coast Media FC wamefanya maandamano ya amani mjini Mombasa kuadhimisha siku ya Uhuru wa wanahabari duniani. Wakizungumza katika shule ya Mombasa Baptist baada kutoa mafunzo ya kitaaluma pamoja na kupanda miti wanahabari wameshutumu matukio yanayokiuka Uhuru wa wanahabari nchini wakisema mwaka jana baadhi ya wanahabari walijipata katika hali Tete. Kupitia katibu mkuu Brian Otieno wanahabari hao wametaka serikali kuwachukulia hatua wale wanaokiuka haki za wanahabari. Aidha wanaharakati wametaka hamasisho zaidi ili kuhakikisha wakenya wametambua haki na uhuru wa wanahabari.