Maafisa polisi 4 washtakiwa kwa mauaji ya ‘Baby Pendo’ mwaka wa 2017

  • | Citizen TV
    1,483 views

    Maafisa wanne wa Polisi wameshtakiwa kwa mauaji ya Mtoto Samantha Pendo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017. Miongoni mwa wanaokabiliwa na mashtaka ni maafisa wawili wa ngazi za juu waliokuwa wakisimamia oparesheni Kisumu wakati huo. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ameidhinisha mashtaka dhidi ya wanne hawa huku akifuta mashtaka dhidi ya washukiwa wengine sita.