Maafisa wa kliniki watoa makataa ya siku 21 kwa wizara na serikali kutekeleza makubaliano au wagome

  • | Citizen TV
    185 views

    Chama cha maafisa wa kliniki kimetoa makataa ya wiki tatu kwa wizara na serikali kutekeleza makubaliano kulingana na maazimio yaliyoafikiwa baina yao na waajiri wao katika kaunti ya Kericho. Wafanyikazi hao wa afya wameonya kushiriki mgomo mwaka ujao, iwapo serikali haitatua masuala yanayowasibu yakiwemo kupandishwa vyeo, mazungumzo mapya ya kuafikia mkataba wa maelewano na muundo wa kamati za huduma za afya ya kimsingi