Maafisa wa NG-CDF wawarai wananchi kujitokeza

  • | Citizen TV
    273 views

    Maafisa wa hazina ya ustawi wa maeneo bunge (NGCDF), wamewaomba wananchi kote kujitokeza kwa wingi kutoa maoni kuhusu mjadala wa kuondolewa kwa hazina hiyo. Hii ni kufuatia uamuzi wa mahakama kuwa NGCDF ni kinyume na sheria. Wakizungumza walipozindua miradi iliyojengwa na hazina hiyo katika shule ya upili ya Nyaisa kaunti ya Nyamira, maafisa hao wamesema hafla za kukusanya maoni zitaandaliwa katika ofisi za maeneo bunge yote nchini kuanzia Jumatatu wiki ijayo.Aidha wabunge hao wanasema hazina hiyo ni muhimu kwa miradi ya maendeleo na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kote nchini.