Maafisa wa polisi wafumaniwa wakila mlungula

  • | KBC Video
    3,054 views

    Maafisa kutoka tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC wamewakamata maafisa watatu wa polisi wa trafiki wanaohudumu katika mzunguko wa Globe Cinema jijini Nairobi kwa kupokea hongo kutoka kwa waendeshaji magari. Kulingana na EACC, maafisa hao kwa majina Oscar Serem Biwott, Simon Kiplagat na Edwin Benedict walifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 48,250 katika kipindi cha saa mbili pekee kutoka kwa madereva wa magari ya uchukuzi wa umma na waendeshaji pikipiki. Msako huo uliofanywa na makachero wa tume hiyo, uliwezesha kunaswa kwa fedha hizo na maafisa hao kutoka kituo cha polisi cha Central kukamatwa na kupelekwa katika makao makuu ya EACC ambako waliandikisha taarifa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive