Maafisa wa upepelezi wafika eneo alipopigwa risasi mbunge wa Kasipul Charles Were

  • | Citizen TV
    6,510 views

    Viongozi wa kisiasawanazidi kufika katika makazi ya mbunge wa Kasipul Ongondo Were katika mtaa wa Karen, hapa jijini Nairobi kufariji familia ya marehemu. Tayari maandalizi ya mazishi yameanza huku kamati ya mazishi ikiundwa. Viongozi hao wameongozwa na gavana wa Homabay Gladys Wanga na wabunge kadhaa. Charles Ong'ondo Were aliaga dunia jana baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana hapa jijini Nairobi. Tunaungana naye seth olale moja kwa moja kwa mengi zaidi.