- 1,138 viewsDuration: 3:08Katika eneobunge la Magarini, kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo hilo pia zimefikia kikomo huku vyama vikiendelea kutia bidii kuwashawishi wapiga kura. Mbunge wa Nyali mohammed Ali aliongoza misururu ya mikutano ya kumpigia debe mgombea wa DCP Stanley Karisa Kenga. Kikosi cha ODM kikiongozwa na naibu kinara Abdulswamad Sharif Nasir na gavana wa Kilifi Gedion Mungaro nao walinoa makali ya mwisho.