Magavana wamkosoa Waziri Nakhumicha kwa kutowahusisha kwenye miswada ya afya

  • | Citizen TV
    488 views

    Baraza la magavana limemkosoa Waziri wa afya Susan Nakhumicha kwa kuwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu afya bila kuwahusisha. Magavana waliofanya kikao na Nakhumicha wanasema kuwa baadhi ya vipengee ambavyo vinahusu ukusanyaji wa fedha za hazina ya matibabu, uwazi wa data za wakenya walioko chini ya mpango huo, gharama kwa serikali za kaunti na sheria kuhusu afya zinazotekelezwa na serikali kuu kuwa na nguvu kushinda za kaunti zina utata. Kwa upande wake Waziri Nakhumicha amewahakikishia magavana kuwa mchango wao utazingatiwa katika miswada hiyo kabla ya bunge kuijadili na kupitisha kuwa sheria.