- 1,763 viewsDuration: 1:41Huku magenge ya wahalifu yakionekana katika maeneo mbalimbali humu nchini, wafanyabiashara katika kaunti ya Kilifi wameitaka wizara ya usalama kuimarisha usalama katika maeneo yao ya biashara. Wafanyabiashara hao wanadai kuwa hulazimika kufunga biashara zao mapema kutokana na hofu ya luvamiwa na magenge ya vijana maarufu Panga Boys. Wakizungumza na wanahabari mjini Kilifi wafanyabiashara hao wanadai kuwa ukosefu wa ajira ni mojawapo ya hali zinazowachochea vijana kujiingiza kwenye uhalifu . wameitaka serikali kubuni nafasi zaidi za ajira hasa kwa vijana.