- 3,257 viewsDuration: 3:12Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen sasa anasema kuna magenge mia moja nchini pamoja na maelfu ya wahuni wanaovuruga amani kwenye mikutano ya siasa. Murkomen akiendelea kuwalaumu wanasiasa kwa kuendelea kuwafadhili vijana wanaojihusisha na makundi hayo. Murkomen pia amesema kuwa watu 14 kati ya 17 waliomvamia na kumjeruhi seneta wa vihiga Godfrey Osotsi wametorokea nchi jirani na sasa wanasakwa.