Mahakama kuu yatarajiwa kutoa uamuzi kuhusiana na kesi inayopinga ushindi wa gavana Gladys Wanga

  • | Citizen TV
    426 views

    Mahakama kuu kaunti ya Homa Bay inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusiana na kesi inayopinga ushindi wa gavana Glady's Wanga. Mahakama mwezi uliopita ilikamilisha kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na aliyekuwa mgombea Ugavana wa Homa Bay Evans Kidero. Kwenye kesi hiyo, Kidero anasema kuwa uchaguzi huo uliompa Wanga ushindi ulikumbwa na udanganyifu na kutaka mahakama kubatilisha ushindi wake. Kidero pia aliwashtaki IEBC, Naibu Gavana Oyugi Magwanga, Afisa mkuu wa uchaguzi Homa Bay Fredrick Apopa na chama cha ODM.