Mahakama ya upeo kutoa uamuzi kuhusu kesi ya Seneta Omtatah kupinga Sheria ya Fedha ya 2023

  • | Citizen TV
    979 views

    Mahakama ya upeo inatoa uamuzi wake kuhusu rufaa iliyokatwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah kupinga uamuzi wa mahakama ya rufaa ulioruhusu utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023. kwenye rufaa yake, Omtatah anaitaka mahakama kubatilisha uamuzi wa majaji Mohammed Warsame, Kathurima M’Inoti na Hellen Omondi ulioiruhusu hazina ya kitaifa kuendelea na utekelezaji w ampango wake wa kutekeleza bajeti ya shilingi trilioni 3.6. Omtatah anaitaka mahakama ya upeo kusitisha utekelezaji wa sheria ya fedha unaowatoza wakenya ushuru zaidi hadi pale kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama kuu kupinga uhalali wa sheria hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa. kwenye uamuzi wa mahakama ya rufaa, majaji hao watatu walisema wananchi wangeweza kurejeshewa ushuru wa ziada waliolipa iwapo mahakama kuu itaamua kuwa sheria hiyo ni kinyume na katiba.