Mahakama yabatilisha uteuzi wa watu wanne katika Baraza la Mabadiliko ya Hali ya Anga

  • | Citizen TV
    524 views

    Rais william Ruto amepata pigo baada yamahakama kuu kuwazuia kuingia ofisini watu wanne walioteuliwa kujiunga na baraza mabadiliko ya hali ya anga Jaji Lawrence Mugambi amesema kuwa mchakato wa kuwateua Emily Mwende Waita, John Kioli, Ummar Omar, na George Odera Outa ulikiuka katiba kwani hakuna maoni ya wananchi yaliyotafutwa kuwahusu. mahakama imesema kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa umma ulihusishwa kwenye uteuzi huo kama inavyohitajika kisheria. aidha jaji mugambi ameagiza uteuzi kufanyika upya katika kipindi cha siku tisini.