Mahakama yakubali ombi la Noordin Haji la kuondoa kesi ya ufisadi ya naibu rais

  • | K24 Video
    101 views

    Mahakama ya milimani leo imekubali ombi la mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji la kuondoa kesi ya ufisadi ya shilingi bilioni saba nukta nne dhidi ya naibu rais Rigathi Gachagua na wengine tisa. Kulingana na hakimu Victor wakumile, Gachagua sasa atarejeshewa hati yake ya kusafiria pamoja na shilingi milioni kumi na mbili alizokuwa ametoa kama dhamana.