- 1,000 viewsDuration: 2:17Mahakama Kuu imesimamisha kwa muda amri ya tume ya uchaguzi IEBC iliyomtaka mbunge wa Nakuru Town East David Gikaria kulipa faini ya shilingi milioni mbili unusu kwa kuwahonga wapiga kura eneo bunge la Ol Kalou. Aidha, mbunge huyo bado hajaomba msamaha licha ya kupewa siku mbili kufanya hivyo au apigwe marufuku kuwania wadhifa wowote wa kisiasa.