Mahakama yasimamisha mgomo wa walimu

  • | KBC Video
    48 views

    Mahakama inayoshughulikia kesi kuhusu masuala ya ajira imesitisha kwa muda mgomo wa walimu wa shule za sekondari unaoendelea. Tume ya walimu humu nchini iliwasilisha kesi mahakamani ikidai malalamishi yaliyoibuliwa na walimu hao tayari yameshughulikiwa. Haya yamewadia wakati serikali ikisema walimu wote wa shule za umma humu nchini watapokea nyongeza ya mishahara yao ya miezi ya Julai na Agosti kufikia mwisho wa juma hili. Hali kadhalika wazazi wamehakikishiwa kwamba watoto wao wanaorejea shuleni wako salama licha ya swintofahamu inayoghubika mgomo huo wa walimu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive