MAISHA NA AFYA - WATOTO LAKI 5 WANAZALIWA NA TUNDU KWENYE MOYO AFRIKA

  • | VOA Swahili
    287 views
    Ugonjwa wa tundu kwenye moyo ni tatizo kubwa la kiafaya kwa wagonjwa kutoka mataifa yalio chini ya jangwa la Sahara. Takwimu za shirika la afya duniani zinaonesha kuwa takriban watoto laki tano huzaliwa na hali hii barani Afrika kila mwaka. Wagonjwa wengi hawapati tiba sahihi na wengine hukosa kabisa kutokana na ukosefu wa vifaa na wataalamu wa kutibu magonjwa hayo mapema. Ripota wetu wa Mombasa Amina Chombo amefuatilia jinsi Shirika la misaada la Muntada chini ya mradi wao Little Hearts na madaktari kutoka ulaya wanavyosaidia watoto kutoka jamii maskini barani Afrika kwa kuwafanyia upasuaji. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.