Maiti tatu zimetolewa kwenye vifusi vya jumba lililoporomoka Sagana kaunti ya Murang’a

  • | Citizen TV
    179 views

    Maiti tatu zimetolewa kutoka kwenye vifusi vya jumba lililoporomoka katika eneo la Sagana, kaunti ya Murang'a Jumba hilo la orofa tatu liliporomoka karibu na kituo cha magari cha Sagana jana jioni. Jumba hilo lilikuwa bado linajengwa. Watu watatu waliokolewa hapo jana na kukimbizwa hadi katika hospitali ya rufaa ya Murang'a kwa matibabu. Polisi wanasema maafisa wa uokoaji wameendelea kupekua vifusi hivyo kwa uwezekano kuwa kuna watu wengine ambao huenda wamekwama ndani.