Majangili wavamia maboma tatu na kuiba mifugo huko Ng'aratuko

  • | Citizen TV
    3,591 views

    Kwa mara nyingine tena wezi wa mifugo wamevamia kijiji cha Ng'aratuko, huko Baringo kaskazini na kuiba mifugo siku moja tu baada ya shambulizi jingine kutekelezwa eneo hilo na kusababisha kifo cha mtu mmoja. Shambulizi hilo linajiri huku waziri wa usalama profesa kithure kindiki akitoa agizo kwa maafisa wa usalama kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi wa kisiasa na hata wale wa kidini wanaodaiwa kuhusika na visa vya utovu wa usalama katika maeneo hayo.