Majibizano makali yatarajiwa bungeni alasiri ya leo kuhusu mswada wa fedha 2023

  • | Citizen TV
    449 views

    Majibizano makali yanatarajiwa bungeni alasiri ya leo pale wabunge watakapojadilli mapendekezo ya mswada tata wa fedha mwaka elfu mbili ishirini na tatu. Upande wa Azimio umependekeza mabadiiliko kwa vipengee tata kikiwemo kile cha ushuru wa asilimia 1.5 kwa ujenzi wa nyumba za nafuu na pendekezo la kutozwa kwa asilimia kumi na sita ya ushuru kwa bidhaa za mafuta. Kenya Kwanza umeshikilia kuwa mswada huo ni sharti uidhinishwe kwani utasaidia katika utekelezaji wa ahadi za serikali, jambo ambalo upinzani umeshikilia kuwa hauna ukweli.