- 51,740 viewsDuration: 1:24Victoria Mkwizu, mkazi wa Tabata, amejifungua watoto watano kwa wakati mmoja katika uzazi adimu uliofanyika tarehe 13 Juni 2026. Watoto hao watano, wavulana watatu na wasichana wawili, wamezaliwa salama na wanaendelea kupatiwa uangalizi maalum wa karibu. Uzazi huo ulifanikishwa na jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambao walihakikisha mama na watoto wanakuwa salama katika hatua zote za kujifungua. Je, safari ya Victoria ilikuwaje hadi kufanikisha kujifungua watoto watano? Tazama video hii kujionea simulizi kamili ya tukio hili la ajabu na la kugusa moyo. #bbcswahili #afya ##tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw