- 293 viewsDuration: 2:15Kina mama 74 wanaowakilisha kampuni tofauti tofauti zinazomilikiwa na makundi ya wanawake kutoka kaunti ya Kwale wamefuzu baada ya kupokea mafunzo ya usimamizi wa biashara kutoka kwa Benki ya Equity na serikali ya kaunti ya Kwale . Mafunzo hayo yaliyoendeshwa chini ya mpango wa Fanikisha yanalenga kuwezesha wanawake kupata ujuzi wa kuimarisha bishara zao ili kupata nafasi zaidi za ajira huku wakielimishwa jinsi ya kuchukua na kutumia mikopo ya biashara. Kaunti ya Kwale ina kampuni 200 za wanawake ambazo tayari zinafanya kazi na serikali ya kaunti hiyo kupitia kandarasi mbali mbali.