- 25,641 viewsDuration: 28:21Kampuni ya teknolojia ya Microsoft inasema inaona "ishara za awali za hali kurejea kawaida" kufuatia hitilafu ya kimataifa iliyoanza jana. Hata hivyo, huduma "bado hazijarejea kikamilifu katika hali ya kawaida."Huduma zilizoathiriwa ni zile zinazotolewa kupitia programu za Teams, Outlook, na Copilot. Mamilioni ya watumiaji duniani kote wamepata shida kutuma au kupokea barua pepe. Tovuti ya Downdetector inasema hitilafu ya Microsoft iliathiri nchi 74 duniani, na kuwatatiza zaidi ya watumiaji 28,000. Aidha inasema nchi saba za Afrika ziliathiriwa, huku benki katika nchi kadhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki zikituma taarifa kwa wateja wake kuhusu hali hiyo. Katika taarifa, Microsoft imetupilia mbali uwezekano wa kuwepo kwa shambulio la mtandaoni, ikisema tatizo hilo linaonekana kutokana na masuala ya kiufundi. #microsoft #putin #zelensky #bbcswahili #tiktok #bbcswahilileo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw