- 16,403 viewsDuration: 3:05Mapadre saba wa kanisa katoliki jimbo la Maralal kaunti ya Samburu wametimuliwa kwa muda, huku uchunguzi wa uvunjaji kanuni za kanisa hilo na hata ubadhirifu wa fedha ukiendelea. Askofu wa kanisa hilo katoliki jimbo la Maralal Hieronymus Joya, akitangaza kusimamishwa kazi kwa mapadre hao ambao anasema mbali na kutumia vibaya mamlaka yao kanisani, pia wamevunja sheria kwa kushiriki unywaji mvinyo na hata kuvunja kanuni za kutokuwa na wana wala mahusiano ya kimapenzi.