- 621 viewsDuration: 2:11Aliyekua jaji mkuu ambaye pia ni mwaniaji wa urais kupitia chama cha United Green Movement (UGM) David Maraga amesema serikali inaendesha taifa kwa njia isiyofaa kutokana na uongozi mbaya. Akizungumza katika eneo la Vigurungani eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wakati wa kuhamasisha wananchi kujiandikisha kama wapiga kura, Maraga amesema ufisadi umekithiri katika idara muhimu za serikali akiwalaumu watumishi wa umma kwa kupora mali ya umma. Amesema wizara ya elimu pia inaendeshwa visivyo kutokana na usimamizi mbaya na hali hiyo itaadhiri siku za usoni za taifa hili.