Marekani Jumatatu imeadhimisha kumbukumbu ya 22 ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11.
Mwaka 2001 wakati wa asubuhi, magaidi 19 wa al-Qaida waliteka nyara ndege nne za abiria, na kuzigeuza ni makombora yenye shabaha. Ndege ya kwanza ilianguka katika Jengo la North Tower la Kituo cha Kibiashara cha Kimataifa huko mjini New York. Dakika 16 baadae, ndege nyingine ilipiga Jengo la South Tower. Wakazi wa Manhattan waliyatelekeza magari yao na kuangalia janga hilo likitokea katika jengo lenye ghorofa 110.
Ndege ya tatu iligonga Pentagon, makao makuu ya Wizara ya Ulinzi huko Arlington, Virginia.
Ndege ya mwisho inaelekea ilikuwa ikielekea katika Bunge la Marekani lakini ikaanguka huko Shanksville, Pennsylvania, baada ya abiria kujaribu bila ya mafanikio kuwadhibiti waliokuwa katika chumba cha rubani.
Takriban watu 3,000 kutoka nchi 93 walipoteza maisha yao siku hiyo, shambulizi baya kabisa kutokea katika ardhi ya Marekani tangu shambulizi lililofanywa na Japan katika bandari ya Pearl Harbor mwaka 1941.
#september11 #911 #worldtradecenter
- - - - -
#VOASwahili
Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.