Martha Karua afanya kampeni Mombasa

  • | K24 Video
    253 views

    Mgombea mwenza wa Raila Odinga, Martha Karua amewataka wanawake kupigia kura muungano wa Azimio ambao utashughulikia maslahi yao na kuwapa nafasi za uongozi. Karua amesema hayo katika kikao na kundi la maendeleo ya wanawake katika kaunti ya mombasa hii leo asubuhi. Karua amesema serikali ya Azimio itatimiza ahadi zilizowekwa katika manifesto iliyozinduliwa jana katika uga wa nyayo jijini Nairobi. aidha, amewarai wakenya kudumisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.