Skip to main content
Skip to main content

Maseneta wataka shughuli ya fidia ya maandamano iwe wazi

  • | KBC Video
    71 views
    Duration: 2:52
    FIDIA YA MAANDAMANO Baadhi ya maseneta wanahimiza uwazi kwenye hazina ya shilingi bilioni mbili ya kuwafidia waathiriwa wa ghasia za maandamano, na waliotoweka. Wakigusia taarifa kutoka kwa seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi kuhusu utekelezaji wa malipo hayo maseneta walielezea wasiwasi kuhusu uteuzi wa wanaonufaika, wakitaka orodha kamili itolewe kwa ukaguzi. Mbali na fidia, maseneta hao pia walitoa wito wa utoaji huduma ya ushauri nasaha na kubuniwa kwa vituo vya urekebishaji, wakisisitiza kuwa licha ya pesa kuashiria utu katika mchakato wa mawiano, lengo kuu lazima liwe kukomesha dhuluma za polisi na upatikanaji haki. Msukumo huo umejiri baada ya bunge la seneti kurejelea vikao vyake baada ya likizo ya majuma matatu. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive