Mashambulizi ya Israeli yaua na kujeruhi darzeni za Wapalestina Gaza

  • | VOA Swahili
    642 views
    Wizara ya afya ya Gaza ilisema kulikuwa na darzeni za Wapalestina waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yanayo fanywa na Israeli katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Jumatatu, October 9. Israeli imetangaza vita dhidi ya wanamgambo wa Hamas baada ya kushambulia maeneo ya Israeli yanayopakana na Ukanda wa Gaza. Wapalestina wasiopungua 493 waliuawa katika mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Israeli katika eneo lililozingirwa tangu Hamas ilipoishambulia Israeli Jumamosi, kulingana na idadi ya vifo iliyochapishwa na wizara mapema Jumatatu. Israeli ilisema Jumatatu ilifanya mamia ya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Hamas huko Ukanda wa Gaza, wakati majeshi ya Israeli yakifanya juhudi kuwaondoa wanamgambo wa Hamas ambao bado wanapigana huko kusini mwa Israeli. Msemaji wa jeshi la Israeli Luteni Kanali Richard Hecht aliwaambia waandishi wa habari kuwa mapigano bado yanaendelea katika maeneo saba au nane ndani ya Israeli na ilikuwa inachukua muda mrefu zaidi kuliko ilivyotarajiwa kuzima uvamizi ulioanza Jumamosi. Msemaji mwengine, Luteni Kanali Jonathan Conricus, alisema Israeli ilikuwa imewaita wanajeshi wa akiba 100,000. (Reuters/VOA) #israel #palestine #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas #gazacity #jabila #refugees