- 152 viewsDuration: 1:06Shirika la Undugu Society of Kenya limepaza sauti ya kulilia haki baada ya watoto na vijana wasiokuwa na makazi angalau kumi na watano kuripotiwa kufariki katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Shirika hilo linasema vifo hivyo vinaonyesha mapungufu makubwa katika mifumo ya ulinzi wa watoto nchini na linazitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka.