Mashirika ya kutetea haki yalalamikia kutotekelezwa kikamilifu kwa katiba

  • | K24 Video
    61 views

    Huku taifa likiadhimisha miaka 14 tangu katiba mpya itangazwe rasmi na kuanza kutumika, mashirika ya kutetea haki yanalalamikia kutotekelezwa kikamilifu kwa katiba hiyo ingawa hatua kubwa imepigwa. Mashirika hayo yaliandaa hafla za maadhimisho katika maeneo mbali mbali nchini, yameitaka serikali iwajibike katika kutekeleza haki za kibinadamu na kuwachukulia hatua washukiwa wa ufisadi.