Wanajamii wameungana kuhakikisha wanafunzi wapya walioitwa kuingia gredi ya kumi wanaripoti shuleni wakiwa na mahitaji yote muhimu, katika mfano wa mshikamano wa kijamii unaoongozwa na viongozi wa jamii kutoka mtandao wa Shofco Urban Network (SUN)
Kuanzia makazi duni ya Nairobi hadi miji ya mashambani ya Meru, kaunti ya Kilifi katika eneo la Pwani, viongozi wa SUN waliratibu shughuli za kuchangisha fedha , kampeni za michango na uhamisishaji wa nyumba kwa nyumba kusaidia familia zinazokumbwa na gharama kubwa za kuandikisha wanafunzi katika shule za sekondari