- 273 viewsDuration: 2:18Viongozi wa miungano ya maafisa tabibu nchini wameitaka serikali kuboresha miundo msingi na huduma za afya nyanjani. Wakiongozwa na rais wa muungano wa maafisa tabibu nchini Moses Konde Matole viongozi hao wamesema kuwa ipo haja ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti kuwekeza zaidi katika idara ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora kote nchini huku wakihamasisha wananchi jinsi ya kutumia bima ya SHA.