Mataifa zaidi kutambua Palestina: Israel itasalimu amri?

  • | BBC Swahili
    4,816 views
    Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa uamuzi wa Canada wa kulitambua taifa la Palestina unaweza kufanya mazungumzo ya makubaliano ya kibiashara na Marekani kuwa magumu zaidi. Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz pia amesema kuwa mipango ya kulitambua taifa la Palestina "inawapa ujasiri Hamas na kuimarisha msimamo wake". Canada ni nchi ya tatu ya uchumi mkubwa kufanya uamuzi kama huo katika siku za hivi karibuni. Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney amesema kuwa nchi yake italitambua jimbo la Palestina mwezi Septemba. @MarthaSaranga anachambua suala hili kwa kina usiku wa leo katika Dira ya Dunia TV. Jiunge naye saa tatu usiku kwa matangazo yatakayokujia mubashara kwenye ukurasa wa YouTube wa BBC Swahili #bbcswahili #palestine #israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw