Skip to main content
Skip to main content

Matapeli walenga wasafiri wanaolipa nauli mtandaoni

  • | Citizen TV
    2,390 views
    Duration: 3:23
    Krismasi imewadia, na msafara wa kila mwaka wa wasafiri kuelekea mashinani unaendelea kuwa mrefu huku maelfu ya Wakenya wakisafiri kwa shamrashamra za sikukuu . Hata hivyo, pilikapilika hizo zimewapa mwanya walaghai kuwalenga wasafiri wasio na tahadhari. Abiria kadhaa tayari wamekuwa waathiriwa wa ulaghai mitandaoni. Wahalifu wakijifanya kuwa mawakala wa kampuni halali za mabasi. Maelfu ya kurasa bandia kwenye mitandao ya kijamii zimeanzishwa kuwahadaa wasafiri kwa ahadi za kuwatengea nafasi kwenye mabasi kwa urahisi na haraka.