Naibu Kinara wa Jubilee Fred Matiang’i amemkosoa Rais William Ruto kwa kile alichokitaja kuwa kupuuzwa kwa utekelezaji wa mtaala wa CBE nchini.
Matiang’i amesema mtaala huo unahitaji kuwa na katibu maalum wa kuusimamia ili kuhakikisha serikali inashughulikia ipasavyo changamoto zinazowakumba wanafunzi na walimu.
Wakati huo huo, Kinara wa PNU Peter Munya amesema upinzani utaondoa baadhi ya ushuru unaotozwa Wakenya na serikali, akidai kuwa ni mzigo mkubwa kwa wafanyakazi na wananchi wa kawaida.
Viongozi hao walizungumza katika Kanisa la MCK Makutano, Kaunti ya Meru.