- 1,001 viewsDuration: 34:36Akiwa ameishi na vitiligo tangu alipokuwa na umri wa miaka saba, @clementina_chalamila amepitia changamoto za unyanyapaa, ubaguzi na manyanyaso kutokana na hali yake ya ngozi. Akiwa mtoto, aliitwa majina ya karaha, alitengwa na wenzake na alikua katika jamii iliyokuwa imejaa imani potofu kwamba vitiligo ni ugonjwa wa kuambukiza au husababishwa na uchawi. Leo, amegeuza maumivu yake kuwa dhamira ya kuelimisha jamii na kuwapa matumaini watu wanaoishi na vitiligo na hali nyingine za ngozi. Kupitia taasisi yake ya @beyondskin__initiative, anapinga imani potofu na kuhamasisha jamii kuwakubali na kuwathamini watu wenye hali za ngozi tofauti. @Elizabethkazibure amezungumza naye katika kipindi cha Waridi wa BBC. 🎥 @bosha_nyanje - - #bbcswahili #waridiwabbc #wanawake Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw