Mbunge wa Kuria Mashariki Kitayama Maisori amewarai wenyeji wa Kuria kukumbatia na kushabikia masomo ya mtoto msichana katika jamii.
Akizungumza na walimu, wanafunzi na wazazi, Maisori alisema kuwa uwekezaji katika elimu ya mtoto msichana ni msingi wa maendeleo ya kudumu, huku yakisaidia kuboresha nidhamu, usalama na kufaulu wa wanafunzi. Mbunge huyo alikashifu masuala ya ukeketaji akisema kuwa vitendo hivyo havitatokomezwa kwa nguvu za dola pekee, bali kwa kubadilisha fikra za jamii kupitia elimu bora.