Mbunge wa Mavoko Patrick Makau akamatwa kuhusiana na uharibifu wa Expressway

  • | Citizen TV
    4,884 views

    Mbunge wa Mavoko Patrick Makau amekamatwa mapema leo asubuhi kuhusiana na maandamano ya jana yaliyosababisha uharibifu wa barabara ya Nairobi Expressway. Makau alikamatwa saa kumi alfajiri nyumbani kwake Karen, jijini Nairobi. Maafisa wa upelelezi wa jinai wanamzuilia katika afisi zao zilizoko katika eneo la Kiambu. Waandamanaji waliharibu mali na kuwasha mioto katika maeneo ya barabara hiyo huku wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha. Waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki ameahidi kuwa wahusika wote kwenye maandamano hayo watachukuliwa hatua za kisheria.