Skip to main content
Skip to main content

MCA wa Balambala na maafisa wa zamani washtakiwa kwa kuhusishwa na ufisadi wa malipo ya ksh

  • | Citizen TV
    509 views
    Duration: 1:18
    Tume ya kupambana na ufisadi imewakamata watu watatu wakijumuisha mwakilishi wodi na maafisa wawili wa zamani wa kaunti kwa tuhuma za ufisadi wa malipo ya shilingi milioni 51. Washukiwa hawa waliofikishwa mahakamani mapema leo ni pamoja na mwakilishi wodi ya Balambala Abdi Ibrahim Daar, Aliyekuwa mkurugenzi wa uhasibu wa kaunti Mohamud Dubow Korane na mwanauchumi mkuu wa zamani wa kaunti hiyo Yussuf Bathe Ali. Kwa mujibu wa stakabadhi mahakamani, watatu hawa wanashutumiwa kushirikiana kutekeleza ufisadi kai ya mwezi Aprili na Juni mwaka wa 2022 kwa kuidhinisha malipo kwa kampuni ambayo haikutimiza usamabazaji wa bidhaa na huduma kwa serikali ya kaunti ya Garissa.