Meshack Biwott:''Nilitamani kuwa mtangazaji lakini wazazi walinirai niwe mwalimu''

  • | BBC Swahili
    1,173 views
    Amepata umaarufu wake kwa kuiga sauti za watu mashuhuri mitandaoni, huku video zake zikisambaa mpaka Uingereza. Meshack Biwott anayejulikana kama @arapuria anazidi kuvutia watu kwa ucheshi wake mitandaoni akiwemo mtangazaji maarufu wa kandanda Uingereza Peter Drury ambaye alimtumia ujumbe kuwa angependa wapatane ana kwa ana siku moja. Mwanahabari wetu @judith_wambare alizungumza naye kuhusu safari yake ya kupata umaarufu mitandaoni na pia jinsi alivyoacha taaluma yake ya ualimu na badala yake kuzingatia ucheshi. #bbcswahili #sanaa #kenya