Mfalme Charles wa III apanda mti katika msitu wa Karura

  • | Citizen TV
    1,651 views

    Mfalme Charles wa Uingereza ameyarai mataifa ya ulimwengu kuchukua hatua za haraka kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza katika ziara rasmi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini nairobi , mfalme charles amekiri kuwa eneo la Afrika Mashariki limeathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, huku akihimiza juhudi zaidi za uhifadhi wa mazingira ili kukinga jamii kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.