- 6,869 viewsDuration: 4:19Mfanyabiashara mmoja kutoka Australia anakadiria hasara ya zaidi ya shilingi milioni 77 baada ya kulaghaiwa na watu walioahidi kumuuza kilo 600 za dhahabu. Andrew Gaballa anasema alikuwa ameingia kwenye makubaliano na watu kadhaa wenye uraia wa Marekani na Mkenya mmoja kwamba wangemuuzia dhahabu hiyo na kisha kuisafirisha hadi Dubai. Ila baadaye wahusika walitoweka na fedha zake bila kuwasilisha dhahabu waliokuwa wamekubaliana.