Mzozo kati ya walimu na mamlaka ya afya ya jamii, sha unazidi kutokota huku walimu wa shule za msingi walioko katika chama cha knut wakiipa serikali makataa ya wiki mbili kutatua masuala yaliyoibuliwa la sivyo wagome. Haya yanajiri huku walimu wa shule za sekondari na vyuo anwai walioko chini ya KUPPET wakishikilia msimamo mkali kwamba watasitisha kazi shule zitakapofunguliwa wiki ijayo iwapo wataendelea kutoa ada kabla ya kuhudumiwa hospitalini. Na kama anavyoarifu mary muoki, juhudi za serikali kuzuia mgomo huo zinaonekana kutibuka.