MGOMO WA MADAKTARI
Huduma muhimu za afya zimeathirika pakubwa kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea, ambao sasa umeingia wiki ya nne. Mgomo huu umetokana na mvutano kati ya madaktari na serikali ya Kaunti ya Nairobi. Wakizungumza leo katika Hospitali ya Mbagathi , maafisa wa chama cha madaktari, wamesema kaunti hii haijashughulikia malalamishi yao. Madaktari hao wanataka walipwe mishahara yao iliyocheleweshwa mara moja pamoja na kutatuliwa kwa malalamishi mengine kabla ya kurejea kazini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive