Kitengo cha ujasusi cha idara ya ulinzi nchini Ukraine kimeripoti ugunduzi wa mili miwili zaidi ya wakenya waliosajiliwa na Urusi kushiriki kwenye mapigano yanayoendelea baina ya mataifa hayo mawili. Mili ya Ombwori Denis Bagaka, mwenye umri wa miaka-39 na Wahome Simon Gititu, aliyekuwa na umri wa miaka-31 ilipatikana karibu na mji wa Lyman, katika eneo la Donetsk, nchini Ukraine, ambalo limeshuhudia mapigano makali kati ya wanajeshi wa Urusi na wale wa Ukraine.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive